SWISSAID Publications SWISSAID - SWTA 1 - Kitini cha kilimo hai Uzalishaji wa mazao ya msimu
Published: 20.11.2019
Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. Katika Tanzania zao hili hustawi zaidi katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro. Pamoja na kutoa mafuta vile vile zao hutumika kwa njia nyingine mbali mbali, nazo ni pamoja na: Chakula cha wanyama / mifugo (Mashudu na majani), kurutubisha ardhi na chakula cha binadamu: kutafuna na kuunga kwenye mboga/chakula. Kwa ujumla zao hili hutumika na wakulima kama zao la biashara.