SWISSAID Publications SWISSAID - SWTA 8 - Kitini cha kilimo hai Uhifadhi na usimamizi ya mazao baada_ya kuvuna
Terbit: 20 November 2019
UTANGULIZI
Uhifadhi wa mazao ya kilimo ni hatua ya mwanzo kabisa mara baada tu ya kuvuna.
Hatua zifuatazo huzingatiwa katika uhifadhi bora wa mazao ya kilimo; kuweka mazao
katika hali ya usafi, ubaridi, kuchambua, kutenga katika makundi kulingana na ubora na
kufungasha.
Uhifadhi na usimamizi mzuri wa mavuno kwa kiasi kikubwa huamua ubora wa mwisho,
kujua soko zuri la mazao kulingana na madaraja ya ubora.
Mazao yatokanayo na kilimo yanawezwa kuwekwa katika makundi makuu mawili;
a) Mazao ya nafaka
- Yanajumuisha nafaka pamoja na mazao ambayo mbegu zake hukamuliwa na kutoa
mafuta mfano alizeti, ufuta na karanga.
b) Mazao ya mbogamboga, matunda na mazao yote ambayo yanatokana na mizizi mfano
viazi vitamu, viazi mviringo na mihogo.