この Publication あなたの言語には存在しません, で見る: Kiswahili (sw), English (en),
またはGoogle翻訳を使用する:  

A future worth living for future generations in the project countries and worldwide: this is the goal the staff at SWISSAID works towards every day.  There are 40 people in Berne and Lausanne and about 150 mostly local men and women in project countries. And quite a few partner organisations and patrons, on whose trust we have been building for years.

8 Issues in this Publication (Showing issues 8 - 1)

SWISSAID - SWTA 8 - Kitini cha kilimo hai Uhifadhi na usimamizi ya mazao baada_ya kuvuna - 2019/11/20

UTANGULIZI
 Uhifadhi wa mazao ya kilimo ni hatua ya mwanzo kabisa mara baada tu ya kuvuna.
 Hatua zifuatazo huzingatiwa katika uhifadhi bora wa mazao ya kilimo; kuweka mazao
katika hali ya usafi, ubaridi, kuchambua, kutenga katika makundi kulingana na ubora na
kufungasha.
 Uhifadhi na usimamizi mzuri wa mavuno kwa kiasi kikubwa huamua ubora wa mwisho,
kujua soko zuri la mazao kulingana na madaraja ya ubora.
 Mazao yatokanayo na kilimo yanawezwa kuwekwa katika makundi makuu mawili;
a) Mazao ya nafaka
- Yanajumuisha nafaka pamoja na mazao ambayo mbegu zake hukamuliwa na kutoa
mafuta mfano alizeti, ufuta na karanga.
b) Mazao ya mbogamboga, matunda na mazao yote ambayo yanatokana na mizizi mfano
viazi vitamu, viazi mviringo na mihogo.

SWISSAID - SWTA 7 - Quality Declared Seeds (QDS) - 2019/11/20

Mbegu ni sehem ya mmea ambayo hutumika kuzalisha/kuotesha mmea mwingine, yaweza kuwa ni zao la ua au sehem ya mmea iliyokomaa na kuwa tayari kuendelea kuoteshwa tena, mfano vipando vya muhogo Mbegu ni mojawapo ya pembejeo muhimu katika kilimo. Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora (QDS) ni mojawapo wa vyanzo bora vya mbegu vya kutegemewa na wakulima. Mfumo wa uzalishaji wa mbegu bora za kuazimiwa ubora ulianzishwa na shirika la kilimo na chakula duniani (FAO) mwaka 1993 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2006.

Mbegu hizi ziliingizwa kwenye mfumo rasmi wa kuzalisha mbegu katika sheria ya mbegu ya mwaka 2003, pamoja na kanuni, miongozo na taratibu zake za uzalishaji za mwaka 2007. Mbegu hizi huzalishwa na mkulima mmoja mmoja au kikundi cha wakulima kilichosajiliwa na kupata mafunzo kwa ajili ya kuzalisha mbegu kwa matumizi yao binafsi na/au kuuza kwa wakulima wa maeneo ya jirani. Ni muhimu nasaba/asili ya mbegu hiyo ijulikane na hivyo mbegu ya msingi au iliyothibitishwa kuwa ndizo pekee zinazotumika katika uzalishaji ili kuhakikisha ubora wa mbegu.

Hapa nchini mbegu zilizopevushwa kiasili (OPV) ambazo zinapatikana katika orodha ya taifa ya mimea ndizo zinazoweza kutumika katika uzalishaji wa mbegu za daraja la kuazimiwa ubora na siyo mbegu za kizazi cha kwanza cha mbegu chotara (F1 Hybrids). Mfumo wa mbegu za daraja la kuazimiwa ubora huwawezesha wakulima kupata mbegu bora kwa gharama nafuu na kwa wakati. Mfumo huu wa QDS upo si kwa nia ya kuubadili mfumo rasmi wa uzalishaji mbegu zilizothibitishwa ubora ila kujaza pengo lililoachwa na mfumo rasmi. Ni mfumo unaowahusu wakulima wadogo wadogo walio kwenye vikundi kwa matumizi yao ndani ya wilaya husika.

SWISSAID - SWTA 6 - Kitini cha kilimo hai Benki_za mbegu za jamii - 2019/11/20

Benki za mbegu za jamii ni taasisi zisizo rasmi, zinazoongozwa na kusimamiwa na wakulima au serikali za mitaa na vijiji ambayo kazi ya msingi ni kuhifadhi mbegu kwa ajili ya matumizi ya ndani.

Benki hizi zinapatikana katika maeneo mengi duniani na zimekuwepo kwa miaka mingi zikiwa na lengo la kuhifadhi, kurejesha, kuimarisha, na kuboresha mifumo ya mbegu ya ndani.

Hapa nchini mwamko wa wanajamii kuanzisha na kusimamia benki za mbegu ni mdogo. Benki hizi zilikuwa zinapatikana katika maeneo machache ya Dodoma na Mbeya. Benki hizi zinajulikana kwa majina mbalimbali: benki za mbegu/jeni za jamii, nyumba za mbegu za wakulima, vibanda vya mbegu, vikundi vya kutunza mbegu, ushirika au mtandao wa kutunza mbegu, hifadhi ya mbegu za jamii, maktaba ya mbegu, na benki ya mbegu za jamii.

Wakulima wanaoendesha benki za mbegu za jamii huhifadhi mbegu za mazao ya aina mbalimbali zikiwemo zile zinazolimwa kwa wingi mfano mahindi, mpunga n.k. Pia wanahifadhi mbegu za mazao yanayolimwa kwa uchache kama vile mtama na mazao ambayo walaji wameyatelekeza kama vile viazi vikuu. Mbegu hizi zinaweza kuhifadhiwa kwa kiasi kidogo au kikubwa kulingana na hitajio na upatikanaji wake.

SWISSAID - SWTA 5 - Kitini cha kilimo hai Upatikanaji wa mbegu - 2019/11/20

Mbegu ni moja ya pembejeo kuu za uzalishaji wa chakula. Wakulima duniani kote wamekuwa wakijua jambo hili kwa karne nyingi. Mamilioni ya familia na jamii za kilimo wamefanya kazi ya kuchagua mbegu na kuzitunza kwa ajili ya matumizi ya msimu wa kilimo unaofuata. Hii ndio imeruhusu kilimo kuenea na kukua na kulisha dunia kwa chakula tofauti.

SWISSAID - SWTA 4 - Kitini cha kilimo hai Ufugaji wa kuku - 2019/11/20

A. Matarajio ya mwongozo
Wafugaji wataweza
- Kujenga banda bora la kufugia kuku
- Tengeneza lishe bora
- Tunza kumbukumbu vizuri za ufugaji
- Kutibu magonjwa kulingana na yalivyoelekezwa
- Watafanya uchaguzi sahihi wa ufugaji kulingana na maeneo Yao.
- Kutambua na kudhibiti magonjwa
- Kuwa mabalozi wazuri wa ufugaji kuku kwa mbinu za kilimo hai
B. Uandishi wa mwongozo
- Mwongozo umeandikwa Kwa kulejea nakala mbalimbali za ufugaji pamoja na uzoefu
wa wafugaji wenyewe katika matumizi ya mimea dawa katika kudhibiti na kutibu magonjwa.
- Mwongozo umelenga magonjwa yanayopatikana na yaliyothibika kuwa sumbufu Kwa
walengwa.

SWISSAID - SWTA 3 - Kitini cha kilimo hai Kilimo mseto - 2019/11/20

Ni kilimo kilicho hai, kilimo chenye kuhusishwa na mazingira bora, mfumo wa usimamizi wa maliasili (mfano: misitu) ambao, kwa kupitia mchanganyiko wa miti mashambani au kwenye ardhi ya kilimo, hupanua wigo na kuongeza uzalishaji na hivyo kuongeza uchumi katika ngazi ya familia hadi Taifa na kuongeza faida katika utunzaji wa mazingira katika ngazi zote za watumiaji wa ardhi.

SWISSAID - SWTA 2 - Kitini cha kilimo hai Kilimo cha mbogamboga - 2019/11/20

Mwongozo wa mafunzo y uzalishaji wa mazao ya mbogamboga

 

SWISSAID - SWTA 1 - Kitini cha kilimo hai Uzalishaji wa mazao ya msimu - 2019/11/20

Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. Katika Tanzania zao hili hustawi zaidi katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro. Pamoja na kutoa mafuta vile vile zao hutumika kwa njia nyingine mbali mbali, nazo ni pamoja na: Chakula cha wanyama / mifugo (Mashudu na majani), kurutubisha ardhi na chakula cha binadamu: kutafuna na kuunga kwenye mboga/chakula. Kwa ujumla zao hili hutumika na wakulima kama zao la biashara.