Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM) Publications TOAM 3 - Kitinia cha kilimo hai Ulinzi wa maji na virutubisho kwenye udongo
Limechapishwa: 20-11-2019

Je, Ninahitaji kujua kitu gani kuhusu udongo na maji? Mimea na wanyama wanahitaji maji wakati wote ili wakue vizuri. Uhaba wa maji hupunguza uwezo wa udongo kulisha virutubisho kwa mimea inayokua, hata rutuba iwe nyingi kiasi gani.