นี้ Publication Issue ไม่ได้อยู่ในภาษาของคุณ, ดูใน: Kiswahili (sw),
หรือใช้ Google Translate:  

Wakulima wana fursa ya kuongeza pato na kuimarisha shughuli za ujasiriamali kupitia mbinu mbalimbali ikiwamo kupanda mazao yenye thamani kubwa, kuliko kupanda mazao ya kitamaduni yaliyozoeleka. Hali hii itawafanya pia waachane na kuzalisha kwa ajili ya matumizi ya kawaida tu, na badala yake wazalishe kibiashara. Kujikita kwenye uzalishaji wa mboga na matunda, siyo kuwa kutawezesha kuboresha kipato cha mkulima pekee, lakini pia kusaidia matumizi bora ya ardhi. Matunda kama vile maembe yanaweza kuzalishwa kwenye ardhi ambayo isingefaa kwa ajili ya kilimo cha mahindi. Upandaji wa miti husaidia kuweka uwiano wa kiekolojia kwenye mazingira na kilimo, ukiacha suala zima la kuongeza kipato kwa wakulima.