Jarida la kilimo endelevu Afrika Mashariki
Mkulima Mbunifu (MkM) ni jarida linalotoa elimu ya kilimo. Lengo la MkM ni kuboresha maisha ya kiuchumi, kijamii na kimazingira kwa wakulima wadogo nchini Tanzania kupitia kuongezeka kwa kilimo endelevu cha kiikolojia na kuboresha uzalishaji wa kilimo. Pakua nakala yako ya mwezi huu. Jarida hili linaangazia mbinu mbalimbali za kilimo na ufugaji, teknologia za uhifadhi wa mazao, ili kuepuka uharibifu na upotevu baada ya mavuno. Soma, jifunze, shiriki na kuwa bora zaidi.
127 Matoleo katika Chapisho hili (Inaonyesha masuala 28 - 19) Iliyopita | Kifuatacho
MkM Toleo la 28 - 01-01-2015
Januari, 2015, Toleo la 28
Mkulima Mbunifu (MkM) ni jarida linalotoa elimu ya kilimo.
MkM Toleo la 27
Disemba, 2014, Toleo la 27
Mkulima Mbunifu (MkM) ni jarida linalotoa elimu ya kilimo.
MkM Toleo la 26 - 01-11-2014
Novemba, 2014, Toleo la 26
Mkulima Mbunifu (MkM) ni jarida linalotoa elimu ya kilimo.
MkM Toleo la 25
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa watu wengi, wanapowaza au kubuni kuanzisha miradi ya kilimo ambapo huwaza kuzalisha mazao makuu pekee. Mara nyingi utasikia au kuona watu wakikimbilia kuweka mipango ya uzalishaji wa mazao ya nafaka kama vile mahindi, mchele, mtama, maharagwe na mengineyo kadha wa kadha, kwa ajili ya chakula na hata yale ya kibiashara kama vile kahawa na korosho.
MkM Toleo la 24 - 01-09-2014
Kuna msemo usemao, mwenye juhudi na maarifa siku zote hufanikiwa katika jambo alifanyalo, bali mlegevu mafanikio hujitenga nae. Na anaeshinda siku zote tuzo ni haki yake. Hali hii imedhihirika pia kwa Mkulima Mbunifu. Tangu kuanzishwa jarida la Mkulima Mbunifu, tumekuwa tukishiriki kwa hali na mali katika shughuli za wakulima nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kushiriki maonesho ya wakulima Nane Nane . Kwa mwaka huu, tumepiga hatua kiasi kikubwa kwa kuwa huduma yetu imeweza kutambulika zaidi miongoni mwa jamii ya wakulima na hata serikalini.
MkM Toleo la 23
Katika jitihada za kutafuta namna ya kufikisha ujumbe kwa wakulima wengi zaidi kuhusiana na njia nzuri na sahihi zaidi za kilimo, MkM imeanzisha kipindi cha redio. Kipindi hiki kitasambaza kwa upana zaidi yale ambayo yamekuwa yakiandikwa katika jarida hili. Kipindi hiki cha redio kitakuwa kikiangazia mafanikio ya wakulima na wafugaji katika nyanja mbalimbali. Kipindi cha Mkulima Mbunifu kinarushwa na kusikika kupitia TBC Taifa na TBC Fm kila siku ya jumanne jioni, saa moja na robo hadi saa moja na nusu.
MkM Toleo la 22 - 01-07-2014
Wakulima wana fursa ya kuongeza pato na kuimarisha shughuli za ujasiriamali kupitia mbinu mbalimbali ikiwamo kupanda mazao yenye thamani kubwa, kuliko kupanda mazao ya kitamaduni yaliyozoeleka. Hali hii itawafanya pia waachane na kuzalisha kwa ajili ya matumizi ya kawaida tu, na badala yake wazalishe kibiashara. Kujikita kwenye uzalishaji wa mboga na matunda, siyo kuwa kutawezesha kuboresha kipato cha mkulima pekee, lakini pia kusaidia matumizi bora ya ardhi. Matunda kama vile maembe yanaweza kuzalishwa kwenye ardhi ambayo isingefaa kwa ajili ya kilimo cha mahindi. Upandaji wa miti husaidia kuweka uwiano wa kiekolojia kwenye mazingira na kilimo, ukiacha suala zima la kuongeza kipato kwa wakulima.
MkM Toleo la 21 - 01-06-2014
Kuku kama ilivyo kwa mifugo wengine, wanahitaji kuwa na banda, na kupatiwa matunzo sahihi. Kwa kufanya hivyo, utaweza kufahamu maendeleo ya mifugo yako na pia kujipatia faida kadhaa zinazotokana na ufugaji wenye tija. Moja ya faida hizo ni pamoja na mbolea, mayai, na idadi ya kuku wako kuongezeka. Ni hatari sana unapofuga kuku kiholela kwani hupotea ovyo kwa kuliwa na wanyama porini, wezi, kutagia porini sehemu ambayo huwezi kupata mayai kwa ajili ya chakula na hata kuuza. Pia, wanaweza kufa kutokana na magonjwa ya aina mbalimbali.
MkM Toleo la 20
Afya bora ni muhimu kwa uzalishaji, na ukuaji mzuri wa watoto. Hili ni lazima lifahamike dhahiri na kila mmoja wetu kuzingatia afya bora kwa ajili ya familia na ukuaji wa taifa. Katika ngazi ya familia, jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa wanazalisha au kununua chakula chenye virutubisho vya kutosha. Wakulima ni lazima kuhakikisha kuwa wanazalisha chakula bora cha kutosha ambacho kitatosheleza mahitaji ya virutubisho kwa ajili ya familia. Ni vyema kuzingatia uzalishaji wa vyakula vyenye protini, tofauti na kuzalisha vyakula vya wanga kama vile mahindi na mchele peke yake.
MkM Toleo la 19 - 01-04-2014
- Uharibifu wa misitu husababisha umaskini
- Tahadhari! Mlipuko wa viwavi jeshi
- Molasesi una faida kwa uzalishaji wa mazao
- Kupe wanahatarisha afya ya mifugo
- Fahamu ugonjwa wa kiwele na matiti unavyoathiri ng’ombe
- Teknolojia muafaka kwa ufugaji wa nyuki
- Boresha pato na afya ya familia yako kwa kuzalisha bilinganya